18 Agosti 2012 - 19:30

waumini wa kiislam wa madhehebu ya shia na sunni leo wamesali ibada ya sunna ya Eidil fitr kote ulimwenguni.

Waumini wakiislam wa madhehebu ya Shia na Sunni kwa pamoja leo wameswali sala ya Eidil Fitr katika masjidul Ghadir iliyoko Kigogo jijini Dar es salam, ambapo ibada hiyo iliongozwa na Sheikh Hamid Jalala. Sheikh Jalala katika hotuba yake alisisitiza kunako kumcha Allha na kujitenga na maasi na kuendelea hivyo kama ilivyokuwa katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.aidha alieleza kuwa matatizo yote yaliowakumba waislamu ni kwasababu wameacha mafunzo ya uislamu na kuwafuata Ahlul Bayti(a.s) kwani wao ndiyo muimili mzima wa uislamu

yafaa kuashiria kuwa sala Eid ya mwaka huu 2012  imesaliwana waumini woote wa kiislam kwa siku moja, tofauti na hapo kabla ambapobaadhi ya makundi ya waislam wamekuwa wakiwatangulia wengine kwa siku moja.

ABNA inakutakieni Eid mubaarak nyote kwa ujumla