12 Septemba 2012 - 19:30

Televehen ya Al alam: waandamanaji wenye asira nchini Yemen wavamia ubalozi wa marekani nchini humo, katika kupinga filamu yenye kumvunjia heshima Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w) na uislamu kwa ujumla

Iliendelea kutangaza kuwa: waandamanaji hao baada ya kufanikiwa kuingia ndani ya ubalozi huo na baada  muda mchache ulionekana ubalozi huo umeshika moto.Baada ya waandamanaji kuingia ndani ubalozi huo Jeshi la usalama nalo liliingia katika ubalozi huo na kuanza kurusha risasi kwalengo la kuwatawanya katika ubalozi huo ambapo watu kadha wamejeruhiwa katika vurugu hizo.Maandamano ya wayemen hao yalianza asubuhi yaleo, kwaajili ya kupinga kuzalishwa kwa filamu inayomtusi mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w) na uislamu kwa ujumla, ambapo waandamanaji hao walikusanyika mkabala na ubalozi huo.