24 Septemba 2012 - 20:30

Rais wa jamhuri ya kiislam ya Iran Dokta Mahamud Ahmad Nejad amesema: tumejiandaa kikamilifu kuilinda dola ya kiislam na wala hatutetereshwi na vitisho vya utawala dhalimu wa Israel

Dokta Mahmud Ahmad Nejad ameya sema hayo alipokuwa akitoa hotuba katika ukumbi wa Umoja wa mataifa. yafaa kuashiria kuwa utawala dhalimu wa Israel umekuwa ukijitutumua kutoa vitisho vya kuishambulia Iran jambo ambalo linaonekana kama kibwagizo kwa serikali ya Iran kwani inaamini kuwa Israel haina uwezo wa kusimama ulingoni na Jamhuri ya kiislam ya Iran.