30 Septemba 2012 - 20:30

Mahakama kuu ya Misri ikiongozwa na Abdussalam Najari leo inachunguza maombi ya mawakili wa Mubaraka kunako kusamehewa kwake

Mawakili wawili wa Husni Mubaraka wametoa maombi kwa hakimu mkuu wa Misri na kumtaka achunguze katika ombi lao la kusamehewa Mubaraka, mawakili hao pia wameomba aachiwe huru haraka kutokana na hali mbaya ya afya yake aliokuwa nayo.Katika hali hiyo hakimu mkuu wa Misri amesema alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari nchini humo kwa kusema: Husni Mubaraka Rais wa zamani wa nchi hiyo hukumu yake itatolewa akiwa katika hospitali ya wafungwa  naye hatasamehewa.Inasemekana Husni Mubaraka amehukumiwa kifungo cha maisha na mahakama ya jinai nchini humo.