Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA- Telesheni ya Al-Jazeera Sport imeeleza kua; Kama ilivyokuwa kawaida imezoweleka kua kufumbia macho mambo yanayotokea ni mchezo wa wanasiasa ila leo hii imeoneka kua mchezo huu umekua maarufu hata katika Shirika la Kandanda Duniani FIFA kukalia kimya kwa muda mrefu kwa mambo wanayofanyiwa wanamichezo wa nchi ya Palestina hasa ukanda wa Ghaza kama kushikwa wanamichezo bila kosa lolote lile na kuvunjiwa viwanja vya kandanda.
Uwanja ulovunjwa uliondoka na Mtoto mmoja alokuwa mchezaji maarufu wa uwanja huo.
Baada ya kushitaki nchi nyingi kunako suala hilo na kukalia FIFA kimya suala hilo mwisho wake FIFA imejitowa kimasomaso kusema kua; Ipotayari kusaidia kuujenga uwanja huo.
Ila la ajabu ni kwamba kujenga uwanja kunafaida gani?! kwani ni lazima kushitaki FIFA Israel kwa kitendo kichafu hicho, kujenga uwanja wa Ashiria kua FIFA haina la kufanya na haina jukumu lolote lile na yaruhusu Israel kufanya hilo kwa mara nyingine tena.
FIFA ni sawa na vyama vya kisiasa vyengine fofauti tu FIFA haipo kisiasa ila malengo yao ni mamoja.