Televisheni ya taifa ya Syria kimeinukuu wizara ya mambo ya ndani ya nchi hiyo ikisema, mifuko 10 ya mabaki ya miili ya watu imekusanywa. Milipuko hiyo imesababishwa na mabomu mawili yaliyotegwa kwenye magari na mabomu mengine mawili ambayo yalilipuka kwa mfululizo katika maeneo tofauti ya Jaramana nchini humo na kufanya uharibifu mkubwa.
Jamarana, kitongoji chenye waumini wengi wa dini ya kikristo na Druze, imeshuhudia mfululizo wa milipuko katika miezi kadhaa iliyopita, kuonyesha jinsi vurugu za kidini zinavyoendelea nchini Syria, nchi ambayo imekumbwa na mgogoro uliodumu kwa miezi 20 sasa.
Milipuko hiyo ililenga kupunguza shinikizo dhidi ya waasi waliozingirwa na jeshi la serikali katika eneo la Daraya, mjini Damascus.
Serikali ya Syria imesema, jeshi la serikali inapambana na wapiganaji zaidi ya elfu moja wa kundi la Al-Qaeda katika maeneo mbalimbali nchini humo.