27 Desemba 2012 - 20:30

Jeshi la ulinzi wa mapinduzi ya Jamhuri ya kiislam ya Iran, Ijumaa ya leo imefungua rasmi mazoezi ya jeshi la maji kuashiria uwezo wake katika nyanja na mbinu tofauti za ulinzi.

mazoezi hayo yanelenga kuonyesha uwezo wa Jeshi la Iran katika kulinda mipaka yake ya maji na kulinda Jamhuri ya kiislamu kwa ujumla  kamanda wa jeshi la maji Jeneral Amir Daryadar mara tu baada ya ufunguzi wa Luteka hii ameashiria akisema: Luteka hii itafanyika katika mlango bahari wa Hormoz,bahari ya Oman,kaskazini mwa bahari ya hindi na ghuba ya Aden.  Opareshen hii imepewa jina la "Ya Husein"  ikiwa na maana "tunaitikia wito wako Husein" ambapo Husein ni kiongozi wa tatu wa waislamu wa dhehebu la Shia ambaye pia ni mjukuu wa mtume Muhammad s.a.w.   mazoezi haya licha ya kukusanya kamandi za makomandoo wa majini pia imekusanya makomandoo wa jeshi la Ardhi na Anga.Jeneral Amir Daryadar aliongezea kwa kusema: lengo letu hasasi la kufanya manuva hii ni kuonyesha uwezo wetu wa kulinda Jamhuri ya kiislam ya Iran pia kuonyesha nafasi yetu katika suala zima la amani ya mashariki ya kati pia ni ujumbe wa amani kwa majirani zetu na wapenda amani wote duniani.pia ameelezea kuwa maadui wa Iran wafahamu kuwa Jeshi la Iran halifanyi mzaha katika suala zima la ulinzi wa Jamhuri ya kiislam ya Iran.yafaa kuashiria kuwa manuva hii itaendelea kwa muda wa siku sita.