3 Februari 2013 - 20:30

Idadi ya watu walio uwawa mkabala na ikulu ya Rais wa jamhuri ya Misri kuanzia asubuhi yaleo imeongezeka nakufikia watu wawili

Shirika la habari la Ahlul Bayt(a.s)-ABNA: idadi ya waandamanaji waliofariki kufikia watu wawili ambapo wamefariki  kabla ya adhuhuri ya jumatatu mkabala na ikulu ya Rais wa jamhuri ya Misri mjini CairoWatu hao walifariki katika vurugu zilizotokia baina ya polisi na waandamanaji mkabala na ikulu hiyo nchini Misri.Kwamujibu wa ripoti hii idadi ya watu walifariki kwamuda wa wiki moja kufikia watu 58, maandamano hayo bado yanaendelea  baina ya jeshi la polisi na waandamanaji katika barabara za mjini Cairo vilevile karibu na chuo kikuu cha kiamerika, ambapo majeshi ya polisi kwaajili ya  kuwatawanya waandamanji hao wamelazimika kutumia mabomu ya machozi na kuwafyaturia risasi waandamanaji hao , kwa upande wa  waandamanaji nao wakitumia mawe kuwarushia wana ulinzi hao.