Ripoti ya Shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA- Taarifa kutoka ofisi ya Papa yaeleza kua, hatua hiyo imetokea tu baada ya kuendelea kudhoofika kiafya kiongozi huyo Katoliki.
Papa Benedict XVI mwenye umri wa miaka 85 alichaguliwa kuongoza Kanisa la Katoliki 19/4/2005 baada ya kuaga dunia Papa John Paul II.
Pamoja Vatican imeeleza kua sababu ya kujiuzulu kiongozi huyo ni umri wake kuwa mkubwa, wachambuzi wa habari waeleza na kuamini kua tuhuma na kashfa mbalimbali ambazo ndio chanzo cha kuchukua hatua, hasa tuhuma za Viongozi wa Kanisa la Katoliki kulawiti Watoto wagodo, aidha hiyo ni miongoni mwa sababu za kulazimika kuchukua uamuzi huo.
Papa Benedict XVI ni kiongozi wa pili wa kanisa katoliki kujiuzulu kutoka katika wadhifa wake, Mwaka 1296, Celestine V aidha alijiuzulu kutokana na sababu zisizojulikana ila sababu kuu ilikua ni kudhoofika kiafya.
Kwa mara hii Kanisa la Katoliki litajitahidi kuchagua Kiongozi mwenye afya njema ili isijetikea mambo kama haya ya kudhalilidha Kanisa.
Tafakari, Uongozi wa Kiislamu huna mambo kama haya, tazama selikali ya Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran yaongozwaje, serikali hiyo yaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za Mwenyezi Mungu na si mtu kujisikia muda wowote kujiuzulu au kujitowa la hasha kukubali uongozi ni kula kiapo na Mwenyezi Mungu kuongoza umma hutoachia ngazi ya uongozi mpaka mwisho wa pumzi yako ya mwisho. Hii ndio tofauti ya Dini Tukufu ya Uislamu na Dini nyengine.