12 Februari 2013 - 20:30

Kuzuiliwa kuingia nchini Libya kila pasipoti iliokuwa na viza ya Iran, suala hili limebainika baada ya ubalozi wa Lebanon nchini Libya kutangaza kuwa kila pasipoti ya mlebanon iliokuwa na viza ya Iran hataruhusiwa kuingia nchini Libya

Shirika la habari la AhlulBayt(a.s)-ABNA: serikali ya Libya imepitisha hukumu yakuwa kila mwarabu na wageni wote kuzuiwa kuingia nchini humo endapo pasipoti zao zitakuwa na viza ya kuingia Iran.Pia inanukuliwa kuwa wafanyakazi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa nchi hiyo imewarejesha watu wenye pasipoti zenye viza za kuingia katika jamhuri ya kiislamu ya Iran.Hali hii imefahamika baada ya ubalozi wa Lebanon nchini Libya kuwahabarisha watu wake kuwa walibanon ambao walisafiri nchini Iran na pasipoti zao kuwa na viza ya kuingia Iran hawaruhusiwi kuingia nchini humo. Inasemekana kuwa vyombo vya habari vya nchini humo hasa magazeti kila siku kukicha vinasisitiza kujieposha na fikira za kishia ziliopo nchini humo.