Taarifa iliyotolewa jana na Shirika hilo imesema, watu 9,300 walifariki katika maafa 310 yaliyotokea duniani mwaka jana, na zaidi ya watu milioni 100 wameathiriwa na maafa hayo.
Mkurugenzi wa UNISDR Elizabeth Longworth amesema, maafa mengi yanaweza kuepukwa mapema. Pande mbalimbali zinapaswa kushirikiana kwa pamoja na kujenga mtandao wa kimataifa ili kupunguza hasara zinazotokana na maafa.