Shirika la habari la AhlulBayt(a.s) –ABNA; siku ya jumapili asubuhi muda wa saa nne kulitokea mlipoko wa bomu katika sherehe za ufunguzi wa kanisa katoliki mjini Arusha, ambapo mgeni rasmi katika sherehe za ufunguzi wa kanisa hilo alikuwa ni muakilishi wa papa Tanzania; Askofu Mkuu Francisco Montecillo na balozi wa vatican nchini Tanzania.
Katika tukio hilo mtu mmoja alifariki papo hapo na wengine 59 kujeruhiwa akiwemo balozi wa Vatican nchini Tanzania na majeruhi hao wakiwa na hali mbaya na kulazwa hospitali, inasadikiwa kuwa katika majeruhi hao wane wako mahutiti.
Kamanda wa Polisi mjini Arusha amelezea tukio hilo kuwa ni la kigaidi kwa sabu aliyekuwa amerusha bomu hilo alikuwa amemlenga balozi wa Vatican pamoja yakuwa hakufanikiwa kutokana na wingi wa watu walikuwa katika hafla hiyo, kamanda huyo alisema kuwa wataalamu wa mabomu wa masuala ya mabomu katika jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) wanachunguza aina ya bomu hilo.
Tukio hilo limetoke balozi wa Vatican akiwa amesimama akiwa na mwenyeji wakeAskofu Mkuu, Josephat Lebulu, mapadri na watawa kutoka mashirika mbalimbali ya Jimbo Kuu la Arusha kwa ajili ya kukata utepe wa uzinduzi, Kamanda Sabas alisema mtu aliyerusha bomu hilo alitokea nyuma ya kanisa hilo la ghorofa na kurusha bomu hilo kwa mkono wa kulia... “Alifanya jitihada za kupenya ili awafikie viongozi lakini alishindwa kutokana na wingi wa waumini waliokuwapo kwenye eneo hilo.”
Rais wa jamhuri ya mungano wa Tanzania mheshimiwa Jakaya Mlisho Kikwete alishitushwa mno na tukio hilo na kulani vitendo hivyo vya kikatili na kuamuru vyombo vya ulinzi kupanga mikakati ya kuwatia mbaloni watu hao, naye aliwataka wananchi kutulia na kuwaachia vyombo vya usalama kuchunguza waliohusika katika tukio hilo.
Inasemekana kuwa mpaka sasa watu watano wamekamatwa wanaodhaniwa kuhusika na tukio hilo ambapo wane kati yao ni raiya wa Saudi Arabia.