Mapigano hayo yanajiri muda mfupi baada ya mjumbe mkuu wa Marekani William Burns kutoa wito kwa vikosi vya usalama kujizuia kwa kiwango kikubwa katika kukabiliana na maandamano hayo kwa kutumia nguvu.Makabiliano yalifanyika baada ya naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani anayezuru Misri, kuwataka maafisa wa usalama kuhakikisha kuwa wanajitahidi kutuliza ghasia wakati wakijizuia kufanya mauaji yoyote.Burns alikutana na maafisa wa serikali inayoungwa mkono na majeshi na kutoa wito wa kusitisha vurugu.
15 Julai 2013 - 19:30
Msimbo wa Habari: 441520
Mamia ya wafuasi wa kiongozi aliyepinduliwa Misri Mohamed Mursi wamepambana na vikosi vya usalama katikati mwa mji wa Cairo na ambapo polisi waliwafyatulia waandamanaji hao gesi ya kutoa machozi.