ABNA- Shirika la ujasusi linalofuatilia ujumbe wa kigaidi kwenye mtandao wa internet lenye makao makuu nchini Marekani (SITE) limesema, kundi la Islamic State in Iraq and the Levant (ISIL) lilitoa tangazo kwenye mitandao ya kidini likiwataka wapiganaji wake waliopo Baghdad, mikoa ya kusini na kwengineko kufanye mashambulizi katika siku ya tatu ya Eid ili kupinga operesheni iliyofanywa na serikali ya Iraq dhidi ya wapiganaji.
Jumamosi iliyopita, jumla ya mabomu 12 yaliyotegwa kwenye magari yalilipuliwa mjini Baghdad, yakilenga zaidi maeneo ya sokoni, migahawa, na hoteli. Milipuko hiyo ilitokea wakati wa sikukuu ya Eid el Fitr, ilisababisha vifo vya zaidi ya watu 30 na kujeruhi wengine zaidi ya 100.