Ripoti ya ABNA- Kwa upande mwingine, Rais Evo Morales wa Bolivia amemkosoa vikali Rais Barack Obama wa Marekani na kusema kuwa, Obama hawezi kuzungumzia amani na usawa, katika hali ambayo nchi yake inazidhulumu na kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine duniani. Akihutubia kwenye mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Rais Morales ameongeza kuwa, hotuba ya Rais Obama ilikuwa ya kifedhuli na kisafihi na kusisitiza kuwa, kiongozi huyo wa Marekani alihutubia kana kwamba ni mfalme wa ulimwengu mzima.
24 Septemba 2013 - 20:30
Msimbo wa Habari: 466745
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina ameikosoa vikali hotuba ya Rais Barack Obama wa Marekani aliyoitoa New York kuhusiana na kutambuliwa rasmi utawala wa Kizayuni wa Israel. Riyadh al Maliki amepinga vikali pia matamshi ya Rais wa Marekani ya kutaka utawala wa Israel utambuliwe kama nchi ya Kiyahudi na kusisitiza kuwa, matamshi hayo hayakubaliwi katu na wananchi wa Palestina.