Ripoti ya ABNA- Baada ya mazungumzo hayo, Obama amesema ana imani watafikia suluhisho la mpango wa nyuklia wa Iran. Marais hao wawili wamewataka wawakilishi wao kufanya kazi kwa ufanisi na kuendelea kushirikiana na nchi nyingine kwa lengo la kufikia makubaliano kuhusu suala la nyuklia.
Ofisi ya rais wa Iran pia imethibitisha kufanyika kwa mazungumzo hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter. Alhamisi, waziri wa mambo ya nje wa Iran Javad Zarif alikutana na wenzake kutoka nchi za Uingereza, China, Ufaransa, Russia na Marekani kuzungumzia mpango wa nyuklia wa nchi hiyo.