Ripoti ya ABNA- Takwimu zilizotolewa na tume ya Umoja wa Mataifa nchini Iraq zinaonesha kuwa, kuanzia mwezi Januari hadi Agosti mwaka huu, karibu watu 5,000 wameuawa na wengine elfu 12 kujeruhiwa katika mashambulizi ya kigaidi na mapambano nchini Iraq.
29 Septemba 2013 - 20:30
Msimbo wa Habari: 468323
Watu wasiopungua 42 wameauwa na wengine 63 kujeruhiwa katika mashambulizi yaliyotokea jana katika sehemu mbalimbali nchini Iraq. Katika mji wa Mussaiyb kusini mwa Baghdad, shambulizi dhidi ya msikiti limesababisha vifo vya watu wasiopungua 30, na wengine 40 kujeruhiwa.