10 Juni 2014 - 17:56
Sheikh Mohammed Idris wa Kenya Auawa

Sheikh na mhubiri mashuhuri wa kiislamu wa Kenya Sheikh Mohammed Idris ameuawa na watu wasio julikana.

Sheikh Mohammed Idris ameuawa kwa kupigwa risasi leo majira ya Alfajiri akiwa njian kuelekea masjid kwa minajili ya kutekeleza ibada ya Alfajir katika mji wa Mombasa Kenya.
Kamishna mkuu wa polisi wa Mombasa, Marwa amesema kuwa uchunguzi unaendelea ili kubainmisha waliohusika na mauaji hayo na dhamira yao.
Marehemu Sheikh Mohammed Idris alikuwa ni mwenyekiti wa chama cha maimamu na wahubiri wa kiislamu Kenya.