20 Juni 2014 - 15:57
Msikiti wa kwanza wafunguliwa nchini Denmark

Msikiti huo unaukubwa wa mita 6700 za mraba ambapo ujenzi wake umetumia kiasi cha Euro milioni 20 ukiwa msikiti wa kwanza wnye mnara nchini Denmark

Shirika la habari AhuluBayt (a.s) ABNA: shererhe za ufunguzi wa msikiti huo zilifanyika jana nchini humo ambapo hakukuhudhuriwa na kiongozi yeyote wakisiasa wa Denmark nakuwa msikiti wakwanza wenye mnara katika nchi hiyo iliopo barani Ulaya
Eneo la msikiti huo linamita 6700 za mraba naujenzi wake kutumia gharama za Euro milioni 20 ambapo imekusanya sehemu ya msikiti, sehemu ya masuala ya kitamaduni, studio ya TV na ukumbi wa michezo kwa vijana.
Kwamujibu wa mtandao wa habari wa Euronews imetangaza kuwa gharama za matengenezo ya msikiti huo ni Euro milioni 20 ambazo zimedhaminiwa na serikali ya Qatar.
Katika shirehe za ufunguzi wa msikiti huo hakukuhudhuria kiongozi yeyote wa kisiasa nchini humo, aidha kunako utengezaji wa msikiti huo kulikuwa na wengi walipinga nakuto ridhia uenzi wa msikiti nchini Denmark.
Pamoja nakuwepo na vyama kamavile Denmark National Party ambacho kinapinga vikali suala hilo nakuwa na mtazamo mkali dhidi ya waislamu, ama viongozi wa msikiti huo hawazitilii manani pingamizi zao nakusema kuwa zipo mbali na hakika na ukweli.