Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: habari kutoka katika tovuti ya kipalestina (Alfalestina Al-yaum) zaeleza (Ashrafu Al-qudra) msemaji mkuu wa wizara ya Afya nchini Palestina amesema: toka kuanza mashambulio ya kinyama ya utawala wa kizayuni dhidi ya wananchi wa Palestina ambayo yalianza julai 7 katika ukanda wa Gaza mpaka sasa yafikisha idadi ya mashahi kuwa watu 314 na majeruhi kufikia watu 2270.
Kwamujibu wa ripoti hii hali halisi inaonyesha kuwa asilimia kubwa ya waliofariki katika mauaji hayo ni kutoka katika jamii ya watoto na wanawake
Hii nikatika hali ambayo televishen ya Almayadini kabla ya kutolewa ripoti hii ilitoa taarifa ikinukuu kutoka katika vyanzo vya Afya nchini Palestina kuwa miili ya watu watano wapalestina yatolewa chni ya kifusi cah nyumba ilioporomoshwa kwa kupigwa mabumo ya ndege za kivita za kizayuni.
Utawala wa kizayuni uliaza kufanya mashambulizi yakinyama ya Ardhini, anga na bahari katika ukanda wa Gaza dhidi ya wananchi wa wapalestina na mpaka sasa bado wanaendeleza mauaji hayo yakinyama dhidi ya wananchi hao wasiokuwa na mtetezi.