23 Oktoba 2014 - 19:37
Ndege za Marekani zashambulia visima vya mafuta Syria

Ndege za Marekani na washirika wake zimeshambulia visima vya mafuta vya serikali ya Bashar Asad.

Ndege za Marekani na washirika wake zimeshambulia visima vya mafuta vya serikali ya Bashar Asad.
Ndege hizo za kivita zimeshambulia visima vya mafuta vya serikali ya Syria mara mutawalia, huko mashariki kwa Syria.
Majeshi ya Marekani na washirika wake yanadai kuwa yameshambulia visima hivyo, kwa dhana kwamba ndio kitega uchumi cha magaidi.
inaripotiwa kuwa mashambulizi ya Marekani na washirika wake mpaka sasa yamesababisha vifo vya raia wasiokuwa na hatia wapatao 553.
ikumbukwe kuwa Marekani na washirika wake wameanza mashambulizi katika ardhi ya syria tangu tarehe 22 mwezi wa tisa mwaka huu, bila ya kupata idhini ya serikali ya Syria.