Jeshi la Iraq likishirikiana na jeshi la wananchi waliojitolea limeendelea kusonga mbele katika mapambano yake dhidi ya magaidi hatari wa Daesh.
mafanikio haya makubwa yameshuduhiwa katika mji wa Salahuddin ambapo jeshi la Iraq limefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwafukuza magaidi wa Daesh.
Imetimia miezi sita tangu jeshi la Iraq kuanza mapambano dhidi ya magaidi wa Daesh, ambao wamekuwa wakifanya jinai na kuua watu wasio na hatia.
Jeshi la Iraq pia limefanikiwa kutegua mabomu mengi ambayo yalitegwa na magaidi hao, kabla hawajakimbia na kurudi nyuma katika uwanja wa mapambano katika mji huo wa Salahuddin.
Majeshi ya Iraq yameahidi kufanya mashambulizi shadidi, dhidi ya magaidi hao hatari.
25 Oktoba 2014 - 15:25
Msimbo wa Habari: 646747
Jeshi la Iraq likishirikiana na jeshi la wananchi waliojitolea limeendelea kusonga mbele katika mapambano yake dhidi ya magaidi hatari wa Daesh.