Mwanamke wa kiiraq ambaye ametekwa na kundi la kigaidi la Daesh abahatika kupiga simu kwa askari wa Iraq.
Mwanamke huyo alikuwa akiongea na maafisa wa jeshi la Iraq kwa uchungu akisema: tunaomba kama mnajua mahala tulipofichwa, tunaomba mje mpige mabomu na kutuangamiza katika sehemu hii, tumechoka kudhalilishwa.
Aliendelea kuelezea kwa uchungu huku akilia na kusema kwamba: sehemu hii tuko mateka wa kike chungu mzima, kila siku tunabakwa kwa uchache mara thelathini,hivi sasa wengine hatuwezi hata kutembea kutokana na maumivu tulonayo.
Mateka huyo aliendelea kusema kuwa: wenzetu wengine wanachinjwa na wengine wanaamua kujiua kutokana na madhila tunayofanyiwa, tunaomba mtuangamize kwa mabumu, tumechoka kudhalilishwa, kama hamtaangamiza sehemu hii kwa mabomu, basi tutachukua jukumu la kujiua.
Ripoti ya umoja wa mataifa inaonyesha kuwa zaidi ya wanawake elfu saba wametekwa na makundi ya kigaidi huko Iraq.
Daesh ni kikundi cha kigaidi kinachopata himaya na msaada wa silaha na fedha kutoka katika nji za magharibi na baadhi ya nchi za kiarabu, kundi hili linafanya jinai kwa kutumia jina la dini tukufu ya Uislamu.
27 Oktoba 2014 - 08:08
Msimbo wa Habari: 647164
Mwanamke wa kiiraq ambaye ametekwa na kundi la kigaidi la Daesh abahatika kupiga simu kwa askari wa Iraq.