31 Oktoba 2014 - 19:40
Sweden yafungua ubalozi Palestina

Waziri wa mambo ya nje nchini Sweden baada ya kuitambua rasmi nchi ya Palestina amesisitiza kuwa suala hilo linawezekana likaipatia mustakabali bora nchi ya Palestina na Israel.

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: serikali ya Sweden siku iliopita imetangaza rasmi kuwa Palestina ni nchi huru na haki, (Margot Valstrvm) waziri wa mambo ya nje ya Sweden alisema hayo katika makala yake alioisambaza katika gazeti la (DN) nchini humo.
Naye ameandika kuwa: kwakutangaza kuitambua kwetu rasmi nchi ya Palestina bila shaka fungamano letu na serikali ya Israel haitakuwa nzuri, aidha alibainisha kuwa maamuzi ya serikali ya Sweden yamechukuliwa katika hali ngumu na nzito kitaifa.
pia amesisitiza kuwa: yawezekana wengi wakafikiri kuwa maamuzi hayo yamechukuliwa kiholela na haraka, ama khofu tulionayo ni kuchelewa kwetu kufanya maamuzi katika suala hilo, kwani ujenzi unaotakiwa kufanywa hivi karibuni nautawala wa kizayuni wa Israel utaleta hali mbaya ya maisha na amani baina ya utawala wa Palestina na Israel, hatimaye kushuhudia matatizo makubwa baina yao, ama kwa kuitambua rasmi nchi ya Palestina katika serikali ya Sweden ni jambo dogo tunaloweza kuwasaidia Wapalestina katika kuishi maisha ya amani na uhuru baina ya nchi ya Palestina na Israel.
Mnamo mwaka 2009 baadhi ya nchi ziliopo katika umoja wa Ulaya katika kikao cha kuleta suluhu na mapatano baina ya (Palestina na Israel) katika mashariki ya kati ambapo walipitisha suala la kuwepo nchi mbili huru (Palestina na Israel) ama kuhusu utekelezaji wa makubaliano hayo mpaka sasa hakujachukuliwa hatua yoyote ya maana.
Kuchelewa kwa makubaliano hayo kumetokea katika miaka hii ya karibuni ambapo hakukupatikana maendeleo yoyote katika mapatano hayo, na badala yake kutokea machafuko yanayopelekea vifo ya watu wasiokuwa na hatia nchini humo.
Waziri huyo wa mambo ya nje ameandika kuwa ratiba mpya ya utawala wa Israel yakujenga nyumba katika maeneo yanayokaliwa kimabavu na waisrael kuwa suala hilo litafanya makubaliano hayo kuwa magumu hatimaye kuongeza machafuko nchini humo.
Aidha alisisitiza uamuzi tuliofikia hivi leo ni ujumbe ambao unaweza kusaidia kufikia mustakabali nzuri baina ya Palestina na Israel. Naye ameandika kwamba sisi tunakusudia kuihami Palestina kwa kutumia  njia ya kuitambua nchi hiyo rasmi.