9 Novemba 2014 - 14:03
Wanamgambo 70 wa Alshabab wauawa

Mamlaka kusini mwa Somali inasema kuwa wanamgambo zaidi ya sabini wa kundi la Alshabaab wameuawa katika mapigano makali yaliyojiri siku ya jumamosi katika vita vya kukidhibiti kisiwa muhimu cha Kudha.

Katika mapambano hayo wanamgambo wa Alshabab wamedhibiti kisiwa hicho na kudai kuwaua zaidi ya askari hamsini wa jeshi Umoja wa Afrika wanaopambana na Alshabab.
ikumbukwe kuwa vikosi vya wanajeshi wa Umoja wa Afrika vikishirikiana na wanajeshi wa Somalia vimekuwa vikiendesha opareshen ya kutokomeza wanamgambo wa Alshababu, na vimefanikiwa katika oparesheni kadha wa kadhaa lakini bado mapambano yanaendelea.