Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Jenerali Rahili Sharif aliyasema hayo siku ya Alhamisi tarehe 20/11/2014 ambapo ndio siku ya mwisho ya kubaki nchini Marekani na baada ya mazungumzo hayo alikwenda katika obalozi wa Pakistan nchini humo uliopo mjini Washington, aidha aliongeza kusema kuwa: jeshi la Pakistan linafanya doria kubwa ya kijeshi dhidi ya vikundi vya kigaidi na doria hizo zinaendelea ikiwa na lengo la kusambaratisha vikundi vyote vya kigaidi nchini humo.
Naye amesisitiza kuwa: mimi natamka wazi kuwa doria ya kuvisaka vikundi vya kigaidi inashamiri kila kikundi kilichoshika silaha na vya kigaidi bila ya kutafautisha baina ya vikundi hivyo.
Kusisitiza kwa kamanda mkuu huyo wa Pakistan katika kutokuwa na tafauti katika vikundi vya kigaidi ni kwa sababu ya maelezo yenye utata aliyo zungumza Sartaj Azizi mshauri mkuu wa waziri mkuu wa wa Pakistan na masuala ya kimataifa alipokuwa akifanya mahojiano na BBC ya lugha ya Kiurdu.
Mazungumzo ya bwana huyo ambaye ni mtu muhimu katika wizara ya mambo ya nje ya Pakistan alipozungumza katika BBC kunako hali ya vikundi vya wanamgambo wa Pakistan limemsababishia matatizo katika wizara mpaka kulazimika wizara hiyo kutoa tamko na kufafanua hali ya mazungumzo ya msaidizi huyo.
Mshauri huyo wa waziri mkuu inadaiwa kuwa katika mazungumzo yake na BBC alionyesha hali ya kuwa serikali ya Pakistan haina haja ya kuvisambaratisha baadhi ya vikundi vya wanamgambo ambao si tishio kwa serikali ya Pakistan na hakuna haja ya kufanya hivyo, Aidha alisema vikundi ambavyo viko dhidi ya serikali ya Marekani haina maana kuwa ni maadui wa serikali ya Pakistan.
Naye aliyasema hayo katika hali ambayo serikali ya Pakistan ilikwisha tangaza kuwa doria za jeshi la nchi hiyo zitahakikisha kuangamiza vikundi vya wanamgambo na magaidi wote waliopo nchini humo.
Serikali ya Marekani imetoa malalamiko mara nyingi kwa utawala wa Pakistan kuwa kwa nini haitaki kuwasaka wanamgambo waliopo katika mipaka ya Pakistan na Afghanistan.
Katika ujumbe wa wizara ya mambo ya nje ya Pakistan unaokosoa mazungumzo ya msaidizi huyo, msemaji mkuu wa wizara hiyo amesema: maneno ya Sartaj Azizi yanayohusu wanamgambo hao yalikuwa yanaelezea hali ya historia yake na si vinginevyo, kwani jeshi la Pakistan limeanzisha Doria ya kuwasaka magaidi wote bila ya kujali tafauti zao.
20 Novemba 2014 - 21:51
Msimbo wa Habari: 652734
Kamanda mkuu wa jeshi la Pakistan alipokuwa katika msafara wake wa kuonana na viongozi wa jeshi la Marekani mjini Washington alisisitiza kuwa suala la magaidi wa Daesh kamwe hawataweza kuingia nchini Pakistan na Afghanistan