21 Novemba 2014 - 11:11
Bashar Assad :juhudi za kimataifa zinahitajika kupambana na IS

Rais Bashar al Assad wa Syria amesema ushirikiano wa jumuiya ya kimataifa unahitajika kulitokomeza kundi la magaidi wa Daesh, nchini Syria ambalo linalengwa na kampeni ya kijeshi inayoongozwa na Marekani.

  Rais Bashar al Assad wa Syria amesema ushirikiano wa jumuiya ya kimataifa unahitajika kulitokomeza kundi la magaidi wa Daesh, nchini Syria ambalo linalengwa na kampeni ya kijeshi inayoongozwa na Marekani. Assad amenukuliwa na shirika la habari la serikali ya Syria, SANA, akisema makundi ya kigaidi kama la Daesh hayakuchipuka bure, bali ni kutokana na sera za kichokozi za wanaoupiga vita utawala wa Syria. Matamshi ya Assad yanakuja siku chache baada ya Rais Barack Obama wa Marekani kukanusha kuna ushirikiano wowote kati ya nchi yake na utawala wa Assad katika mapambano dhidi ya magaidi wa Daesh. Baadaye leo Makamu wa Rais wa Marekani, Joe Biden, atawasili Uturuki kujaribu kuishawishi nchi hiyo kushirikiana nao katika kupambana na magaidi wa Daesh. Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki amesisitiza kuwa, juhudi za kimataifa zinapaswa kuelekezwa katika kuuangusha utawala wa Assad.

  Yafaa kuashiria kuwa: Uturuki imekuwa ndiyo njia kuu ya silaha na magaidi wanaoingia kupambana na serikali ya Iraq na Syria, Serikali ya Syria imekuwa ikipambana na magaidi kutoka nchi mbali mbali duniani kute, ambapo baadhi wa magaidi hao wanatoka marekani na nchi za ulaya, magaidi hao wanalenga kuondoa utawala wa Bashar asad ambao unaonekana kuwa ni tishio kubwa kwa uwepo wa Israel na maslahi ya Marekani ya Mashariki yakati.

Lebo