Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameishutumu Marekani kwa kile alichokitaja kuwa ni ufidhuli kuhusiana na mzozo wa Syria.
Erdogan amedhihirisha mvutano uliopo kati ya Uturuki na Marekani kuhusiana na mzozo huo. Hali hiyo imekuja siku chache tu baada ya makamu wa Rais wa Marekani Joe Biden kufanya mkutano muhimu na kiongozi huyo wa Uturuki.Uhusiano kati ya nchi hizo mbili umezorota katika miezi ya hivi karibuni kutokana kutofautiana kimaslahi na hikupelekea Uturuki kutotuma jeshi lake ushirikiana na Marekani kupambana dhidi ya Magaidi wa Daesh waliyoteka maendeo makubwa ya Syria na Iran.Erdogan amesema haelewi kwanini mtu atoke zaidi ya kilomita 12,000 kuja katika kanda hiyo kutoa msaada wa kijeshi. Biden alimkera Erdogan kwa kusema sera za Uturuki za kuunga mkono waasi nchini Syria ndizo zilizochochea kuibuka kwa makundi ya kigaidi nchini Syria na Iraq.
Ni muhumu kuashiria kwamba Serikali ya Uturuki imekuwa msaada mkubwa sana kwa magaidi hao wa Daesh na Uturuki ndio njia kuu ya magaidi hao kuingia na kuingiza silaha na kutoa mali walizonyang’ganya katika nchi za Iraq na Syria, pia imesikika mara kwa mara serikali ya Uturuki ikidhihilisha uadui wake wa dhahiri dhidi ya serikali ya Bashar Asad.