21 Desemba 2014 - 08:50
Putin:Hakuna nchi inayoweza kuitisha Urusi

Rais wa Urusi Vradil Putn amesema:mpaka sasa hakuna nchi inayoweza kuitisha Urusi na haitatokea nchi ya kuitisha Urusi.

Rais wa Urusi Vradil Putn amesema:mpaka sasa hakuna nchi inayoweza kuitisha Urusi na haitatokea nchi ya kuitisha Urusi.
aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na vikwazo ilivyowekewa nchi hiyo, Putin aliwaomba wananchi wa Urusi wawe wamoja na wavumilie vikwazo hivi vya muda mfupi.
Urusi imekuwa ikituhumiwa na Marekani na washirika wake kwa kusaidia waasi wa Ukraine ambao wanataka kujitenga na nchi hiyo na kujiunga na Urusi.
ikumbukwe kuwa hapo kabla wananchi wa eneo la Crimetia walipiga kura ya kijitoa katika himaya ya ukraine na kujiunga na Urusi ambapo walipiga kula za kuunga mkono kujiunga na Urusi kwa asilimia 96.8 na hatimaye walijiunga na Urusi, hali hii ilipelekea sehemu nyingine ya Ukraine kutaka kujiunga na Urusi na kufanya harakati za kujitoa katika himaya ya nchi hiyo, lakini jeshi la nchi hiyo lilitumia nguvu kukabiliana na wananchi hao, ndipo wananchi hao walipoamua kushika silaha na kuhatarisha kabisa amani ya Ukraine,baada ya hali ya machafuko kushadidi miji mingine miwili ya Ukraine ilitangaza bayana azma yake ya kutaka kujiunga na Urusi, inahofiwa kuwa huenda miji mingi zaidi ikahitaji kujiunga na Urusi na hata hali hii kusambaa kwa nchi nyingine ambazo zilikuwa katika muungano wa Soviet wa zamani, jambo ambalo linaitisha na kuipa hofu kubwa Serikali ya Marekani.
Kwa sasa Ukraine inaungwa mkono na Marekani na washirika wake na kwa upande mwingine wanaituhumu Urusi kwa kuwaunga mkono wananchi wanaotaka kujitenga na Ukraine, na hii ndio sababu ya Marekani na wafuasi wake kuiwekea Urusi vikwazo kwa lengo la kuidhoofisha kiuchumi.

Lebo