1 Januari 2015 - 11:23
Palestina yajiunga na ICC baada ya Umoja wa mataifa kukataa mswada wake

Rais wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas amesaini mikataba 20 ya kimataifa jana Jumatano, ukiwemo wa Rome uliounda mahakama ya kimataifa ya ICC

Rais wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas amesaini mikataba 20 ya kimataifa jana Jumatano, ukiwemo wa Rome uliounda mahakama ya kimataifa ya ICC, siku moja baada ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kukataa maombi yake kuishurutisha serikali ya Israel kuondoka na kurudisha ardhi ilizozichukua kwa nguvu kutoka kwa Palestina kabla ya mwaka 2017.

Hatua hiyo iliyozikarisha Israel na Marekani, inaisafishia njia ICC kushughulikia uhalifu uliyofanywa katika ardhi za Palestina, na kuchunguza matendo ya viongozi wa Israel na Palestina katika mgogoro huo wa umuagaji damu uliyodumu kwa zaidi ya muongo mmoja.

Abbas aliuambia mkutano wa viongozi wa Palestina katika hotuba iliyotangazwa na televisheni ya serikali, kuwa Israel inawashambulia wao na ardhi yao kila siku, na hawana popote pa kukimbilia kwa kuwa hata baraza la usalama limewangusha.

Israel licha ya kuchukua kwa nguvu  na kudhulumu ardhi na haki za wapalestina, inafanya mashambulizi ya kijeshi mara kwa mara dhidi ya wananchi madhulumu wa Israel na ulimwengu na Umoja wa mataifa unafumbia macho jinai na mauaji yanayofanywa isipokuwa nchi chache tu ndio zinazoonyesha kusikitishwa na mauaji hayo yanayofanywa na serikali ya Israel.

 

Lebo