15 Januari 2015 - 10:27
Wabunge Marekani unga mkono vikwazo zaidi dhidi ya Iran

Wabunge wa vyama vya Republican na Democratic nchini Marekani wataendelea na mipango ya kuiwekea jamhuri ya kiislamu ya Iran vikwazo zaidi

Wabunge wa vyama vya Republican na Democratic nchini Marekani wataendelea na mipango ya kuiwekea jamhuri ya kiislamu ya Iran vikwazo zaidi, licha ya onyo kutoka ikulu ya White House kuhusu hatari ya kukwamishwa kwa mazungumzo ya nyuklia. Wabunge hao wanaohofu kuwa wajumbe wa majadiliano wa utawala wa Obama hawataweza kuchukua msimamo thabiti dhidi ya Tehran, wanaandaa pia mswada tofauti kulipa bunge mamlaka ya kuidhinisha makubaliano yoyote ya mwisho kuhusu mpango wa nyuklia wa jamhuri ya kiislamu ya Iran. Maseneta Mark Kirk wa Republican na Robert Menendez wa Democratic wanakamilisha mswada wa vikwazo vikali zaidi dhidi ya jamhuri ya kiislamu ya Iran, ikiwa hakutakuwa na makubaliano ya mwisho kufikia Juni 30. Kamati ya benki ya Seneti, itafanya kikao kuhusu vikwazo dhidi ya jamhuri ya kiislamu ya Iran Jumanne ijayo, kwa mujibu wa Seneta Bob Corker, mwenyekiti wa kamati seneti ya uhusiano wa masuala ya kigeni. Ikulu ya White House imesisitiza kuwa kupitishwa kwa sheria hizo kunaweza kuilaazimisha jamhuri ya kiislamu ya Iran kujiondoa katika mazungumzo na mataifa sita makubwa.

Marekani, Israel na mataifa ya Ulaya yanaituhumu jamhuri ya kiislamu ya Iran kwa kuwa na mpango wa kutengeneza makombora ya nyuklia jambo amabalo linapingwa vikali na serikali ya jamhuri ya kiislamu ya Iran ambayo inasema kuwa inatengeneza nyuklia kwa malengo ya amani ambayo ni malengo ya kutafuta nishati si kombora, jamhuri ya kiislamu ya Iran inasema kuwa haihitaji kombora la nyuklia kwani inauwezo nguvu za  kukabiliana na adui yake yeyote bila ya kuhitajia kombora hilo.