18 Januari 2015 - 14:25
Israel yataka mahakama ya kimataifa iwekewe vikwazo baada ya kuchunguza jinai zake

Hatua hii ya Israel inaonyesha bayana kabisa kuwa nchi hii inatumia ushawishi wake kuigeuza haki, Israel ni nchi inayoongoza kuwa kufanya mauaji ya kiholela bila ya kuhukumiwa na umoja wa mataifa hii inatokana na utetezi inayoupata kutoka kwa Marekani,Ufaransa na Uingereza.

Israel imesema inafanya mazungumzo na baadhi ya nchi wanachama wa mkataba wa Roma unaounda mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi za uhalifu ICC kuzirai kuipunguzia mahakama hiyo ufadhili baada ya mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya ICC Fatou Bensouda siku ya Ijumma kutangaza kuwa ataanzisha uchunguzi wa awali kuhusu madai kuwa Israel ilihusika katika uhalifu wa kivita dhidi ya Wapalestina, madhila yaliyofanyika kuanzia tarehe 13 mwezi Juni mwaka jana. Waziri wa mambo ya nje wa Israel Avigdor Lieberman amesema nchi yake ambayo si mwanachama wa ICC inatarajia kutatiza ufadhili wa mahakama hiyo unaotoka kwa nchi 122 wanachama. Lieberman ameongeza Israel itazitaka nchi washirika kama Canada, Australia na Ujerumani kusitisha ufadhili wao akidai ICC ni asasi ya kisiasa isiyowakilisha yeyote.

Hatua hii ya Israel inaonyesha bayana kabisa kuwa nchi hii inatumia ushawishi wake kuigeuza haki, Israel ni nchi inayoongoza kuwa kufanya mauaji ya kiholela bila ya kuhukumiwa na umoja wa mataifa hii inatokana na utetezi inayoupata kutoka kwa Marekani,Ufaransa na Uingereza.

Mataifa mengi yamekuwa yakiilaumu mahakama ya kimaifa ya kesi za jinai na uhalifu kwa upendeleo kwani ilikuwa ikizihukumu nchi za kiafrika tu na nchi nyingine dhaifu na kuzifumbia macho nchi kama Marekani, Uingereza, Ufaransa na Israel ambazo zimeendesha vita kadhaa vilivyopelekea kuuawa mamilion ya watu. 

 

Lebo