Serikali ya Japan imesema leo kwamba haitosalimu amri mbele ya ugaidi. Taarifa hiyo inafuatia kutolewa kwa ukanda wa video ukiwaonyesha magaidi wa kundi la Daesh, wakitishia kuwauwa wajapani wawili waliowateka nyara, ikiwa hawatolipwa fidia ya dola milioni 200. Msemaji mkuu wa serikali ya Japan Yoshihide Suga, aliuambia mkutano na waandishi habari mjini Tokyo, kwamba waziri mkuu Shinzo Abe ambaye yuko ziarani mashariki ya kati atazungumza na waandishi habari leo mjini Jerusalem na atavunja sehemu ya ziara yake, ingawa mkutano na rais wa Palestina Mahmud Abbas utafanyika kama ilivyopangwa.
20 Januari 2015 - 11:43
Msimbo wa Habari: 665934
Serikali ya Japan imesema leo kwamba haitosalimu amri mbele ya ugaidi. Taarifa hiyo inafuatia kutolewa kwa ukanda wa video ukiwaonyesha magaidi wa kundi la Daesh