Watu watano wameuwawa leo mjini Mogadishu nchini Somalia katika shambulizi la bomu la kutegwa kwenye gari lililofanywa katika hoteli moja ambako wajumbe wa Uturuki walikuwa wakikutana. Maafisa wawili wa polisi wameuwawa lakini hakuna mjumbe yeyote wa Uturuki aliyejeruhiwa miongoni wa wajumbe 70 waliokuwa ndani ya hoteli hiyo. Kundi la wanamgambo wa al Shabaab limedai kuhusika na shambulizi hilo, lililofanywa siku moja kabla ya ziara ya rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan nchini Somalia. Waziri mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu amesema walizuru Somalia mwaka 2012 katikia mazingira magumu na hawajakata tamaa kuzuru tena nchi hiyo. Davutoglu aidha amesema Erdogan bado anataka kwenda Somalia na alikuwa kiongozi wa kwanza nje ya bara la Afrika kuitembelea nchi hiyo katika kipindi cha miaka 20 alipoizuru mwaka 2011.
22 Januari 2015 - 19:51
Msimbo wa Habari: 666509
Watu watano wameuwawa leo mjini Mogadishu nchini Somalia katika shambulizi la bomu la kutegwa kwenye gari lililofanywa katika hoteli moja ambako wajumbe wa Uturuki walikuwa wakikutana.