Rais wa Ujerumani Joachim Gauck anaendelea na ziara yake nchini Tanzania ambapo leo yupo mjini Arusha. Huko amekutana na rais wa mahakama ya Afrika ya haki za binaadamu Augustino Ramadhani na kisha akaelekea katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano AICC ambapo amefanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Leo mchana Gauck ataelekea mbugani Serengeti ambapo atazindua kituo cha kupambana na uwindaji haramu na pia kufanya mazungumzo na mkuu wa shirika la hifadhi za taifa TANAPA, Allan Kijazi, na mkuu wa shirika la kuhifadhi wanyama la mjini Frankfurt, Christof Schenk.
Tanzania ni moja kati ya nchi za Afrika zenye rasili mali na utajiri wa hali ya juu, ambapo nchi hii inatabiliwa kuwa katika nchi zenye uchumi wa juu barani Afrika katika miaka michache ijayo.