2 Machi 2015 - 18:55
Majeshi ya Wakurdi yapambana vikali na Daesh

Majeshi ya serikali ya Syria na wanamgambo ya Kikurdi yamepambana vikali na kundi la kigaidi la Daesh katika maeneo tofauti leo katika eneo muhimu karibu na mpaka na Iraq na Uturuki.

Majeshi  ya  serikali  ya  Syria  na  wanamgambo  ya  Kikurdi yamepambana vikali na kundi la kigaidi  la Daesh katika  maeneo tofauti leo katika  eneo  muhimu  karibu  na  mpaka  na  Iraq  na Uturuki.

Majeshi  tiifu  kwa  rais Bashar  al-Assad  na  wapiganaji  wa   vikosi vya  ulinzi  wa  umma  vya  Wakurdi  YPG  yamefanya  mashambulizi makali dhidi  ya   kundi la kigaidi  la Daesh katika  jimbo  la  kaskazini mashariki  la Hasakeh.

Mkuu  wa  shirika  linaloangalia  haki  za  binadamu  nchini  Syria Rami Abdel Rahman  ameliambia  shirika  la  habari  la  AFP kwamba  baada  ya  mapambano  ya  siku  tatu , majeshi  ya  serikali yakisaidiwa  na  wapiganaji  kutoka  katika  makabila  ya  Kirabu yamepata udhibiti  wa  vijiji  23  katikati  ya  jimbo   hilo.

Amesema  wapiganaji  wa  kundi  la  YPG pia  wanapambana  na kundi la kigaidi  la Daesh katika  makabila  ya  Waarabu  nje  ya  kijiji  cha  Tal Tamr  katika  eneo  la  kusini  magharibi  ya  jimbo  la  Hasakeh.