3 Machi 2015 - 20:45
 India yaahidi kuimarisha uhusiano na Pakistan

Muungano mpya kati ya chama tawala cha Hindu nationalist na chama cha Peoples Democratic Party, PDP ambacho kinataka utawala huru katika jimbo la Kashmir linalodhibitiwa na India , umetoa ishara kuwa ushirikiano unawezekana.

Mwanadiplomasia  wa  ngazi  ya  juu  nchini  India  ameahidi kuimarisha  uhusiano  na  Pakistan  leo  baada  ya  mkutano  wa kwanza  na  mwenzake  wa  India  tangu  pale  nchi  hiyo  ilipositisha mazungumzo  yenye  lengo  la  kupunguza  mizozo  mingi baina  yao mwaka  jana.

Hali  ya  wasi  wasi  baina  ya  nchi  hizo  jirani  yenye  silaha  za kinyuklia imesababisha  majeshi  ya  nchi  hizo  kufyatua  risasi katika  mapaka  wao katika  jimbo  la  Kashmir  mara  kadhaa  katika muda  wa  mwaka  mmoja  uliopita.

Kiasi  ya  watu  12  wameuwawa  na  maelfu  wamelazimika kukimbia  kutoka  majumbani  mwao  katika  mapigano  ya  hivi karibuni  mwezi  wa  Januari.

Pakistan  na  India  zimepigana  vita  mara  mbili  kuhusiana  na jimbo  la  Kashmir  tangu  mapigano  yaliyofuatia  kugawanywa  kwa nchi  hizo  mbili mwaka  1947 , baada  ya  kumalizika  kwa  utawala wa   kikoloni  wa  Uingereza.