Kamanda wa kijeshi wa kundi la kigaidi Al Nusra lenye mafungamano na mtandao wa Al Qaeda ameuwawa katika shambulio la anga lililofanya na jeshi la Syria kaskazini mwa Syria hapo jana. Kwa mujibu wa Shirika la Kuchunguza Haki za Binaadamu nchini Syria lenye makao yake makuu nchini Uingereza shambulio hilo la ndege za kivita limemuuwa Abu Hamam al -Shamii pamoja na viongozi wengine kadhaa waandamizi wa kundi hilo wakati walipokuwa wakikutana katika jimbo la kaskazini la Syria la Idlib.
Tovuti ya wapiganaji wa jihadi imethibitisha kuuwawa kwa al-Shami na viongozi wengine watatu wakuu wa kundi la Al-Nusra.Shirika la habari la serikali nchini Syria SANA limeripoti kwamba al-Shami na idadi ya wenzake isiojulikana wameuwawa katika operesheni maalum iliofanywa na jeshi la Syria katika kijiji cha al-Habeet nchini humo. Shambulio hilo linakuja siku moja baada ya Al Nusra kushiriki katika shambulio lililosababisha maafa kwenye kambi ya kikosi cha anga cha Syria katika mji wa Allepo kaskazini mwa nchi hiyo.
kundi la kigaidi Al Nusra ni kundi linaloungwa mkono na Israel, Marekani na wafuasi wake kwa lengo la kiiangusha serikali halali ya Syria inayoongozwa na Bashar asad, lakini kundi hilo limeshindwa kuiangusha serikali hiyo kutokana na nguvu za jeshi la Syria, likishirikiana sanjari na jeshi la Iran na Hizbullah.