12 Machi 2015 - 14:15
 Wanajeshi wa Iraq wazidi kusonga mbele katika mji wa Tikrit

Wataalam wa mambo ya kijeshi wanasema kwamba ushindi huu unapatikana kutokana na majeshi ya Iran kuingia kuyasaidia majeshi ya Iraq.

Wanajeshi wa Iraq wanaripotiwa kuichukuwa hospitali ya kijeshi cha Tikrit, iliyo karibu sana na kitovu cha mji huo muhimu unaodhibitiwa na kundi la kigaidi la Daesh lijiitalo Dola la Kiislamu linalopata msaada kutoka mataifa ya magaribi na mataifa ya kiarabu. Kwa mujibu wa meja jenerali mmoja wa jeshi la Iraq aliyekataa kutajwa jina lake, wanajeshi hao waliingia kiunga cha Qadisiya asubuhi ya Jumatano wakiwa pamoja na wanamgambo wa Kishia. Hii ni mara ya kwanza kwa vikosi vya serikali kuingia kwenye mji huo. Hata hivyo, vimeshindwa kusonga mbele baada ya kukabiliwa na mashambulizi ya watunguaji na mabomu ya kutegwa ardhini. Wakati huo huo, wanamgambo wa kundi la kigaidi la Daesh wameanzisha mashambulizi makubwa kuelekea mji wa Ras al-Ayn, wenye wakaazi 50,000 mpakani mwa Syria na Uturuki. Mashambulizi haya yanakuja huku kukiwa na ripoti za wapiganaji wa Kikurdi kuuvamia mji mwengine wa Tal Abyad unaodhibitiwa na kundi la kigaidi la Daesh.

Wataalam wa mambo ya kijeshi wanasema kwamba ushindi huu unapatikana kutokana na majeshi ya Iran kuingia kuyasaidia majeshi ya Iraq.