Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anazungumzia hofu za kushindwa kwa chama chake cha mrengo wa kulia-Likud, katika uchaguzi wa bunge utakaoitishwa wiki ijayo.Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 65 amezungumzia hofu hizo katika hotuba yake kupitia televisheni ya nchi hiyo.Kwa mujibu wa utafiti wa hivi karibuni wa maoni ya umma,muungano wa kati kushoto unaoongozwa na Izhak Herzog utajikingia viti 25 toka jumla ya 120 vya bunge la Israel-Knesset.Chama cha Likud kitajipatia viti 22.Lakini Netanyahu anasemekana anaweza tena kuunda serikali kutokana na uwezekano wa makundi madogo madogo ya mrengo wa kulia kujinyakulia viti vingi bungeni.
Israel kwasasa inakabiliwa na hofu kubwa kuhusu kadhia ya nyuklia ya Iran, na kushindwa kwa magaidi waliowapandikiza Syria kwa lengo la kuiangusha serikali ya Bashar asad.