14 Machi 2015 - 20:28
 Kimbunga kikali chasababisha uharibifu mkubwa Vanuatu

Kimbuga kikali kimepiga kisiwa cha kusini mwa bahari ya Pasifik cha Vanuatu na kusababisha uharibifu mkubwa.

Kimbuga kikali kimepiga kisiwa cha kusini mwa bahari ya Pasifik cha Vanuatu na kusababisha uharibifu mkubwa. Mashirika ya misaada yamesema huenda watu wengi wameuwawa, katika janga hilo miongoni mwa yale mabaya kabisa la  hali ya hewa kuwahi kuonekana katika kanda hiyo. Kiwango hasa cha maafa hakijajulikana  kwa sababu ya kuharibiwa kwa mawasiliano . Kimbuga hicho kilichotokea jana usiku kilikuwa na  kasi ya mwendo wa kilomita 320 kwa saa. Umoja wa mataifa ulikuwa na ripoti zizothibitishwa kwamba watu 44 wamekufa katika mkoa mmoja mapema leo alfajiri, lakini umeshindwa kupata taarifa za idadi kamili  ya waliouwawa na kujeruhiwa katika janga hilo. Hata hivyo uharibifu ni mkubwa.Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Australia Julie Bishop amesema nchi yake  iko tayari kusaidia na ina wafanyakazi wa shughuli za tiba na uokozi waliojitayarisha. Pia New Zealand imetangaza msaada wa haraka wa  dola milioni  moja za New Zeland, ukiwa msaada wa awali kuvisaidia visiwa vya Vanuatu, Fiji , Tuvalu na Solomon.