22 Machi 2015 - 10:43
China, Japan na Korea Kusini zakutana baada ya miaka 3

Mawaziri wa mambo ya nje wa Korea Kusini, China na Japan wamekutana hii leo kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka mitatu mjini Seoul katika juhudi za kutuliza hali ya mvutano katika kanda hiyo kutokana na mizozo ya mipaka na ya kihistoria

Mawaziri wa mambo ya nje wa Korea Kusini, China na Japan wamekutana hii leo kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka mitatu mjini Seoul katika juhudi za kutuliza hali ya mvutano katika kanda hiyo kutokana na mizozo ya mipaka na ya kihistoria. Baada ya mikutano kadhaa ikiwemo ya kujadili uwezekano wa kuandaa mkutano wa kilele utakaowaleta pamoja viongozi wa nchi hizo tatu, wanadiplomasia hao wamekutana kwa mkutano rasmi leo. Mizozo kati ya Japan, China na Korea Kusini ambazo ni nchi jirani kaskazini mashariki mwa bara Asia imetajwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon kama kiunganishi kinachokosekana katika kuleta amani na uthabiti mashariki mwa Asia na Marekani imesema inatiwa wasiwasi na uhasama kati ya washirika wake Korea Kusini na Japan na ingependa kuziona nchi hizo mbili zinashirikiana kukabiliana na ushindani wa matumizi ya mabavu kutoka China.