24 Machi 2015 - 09:09
Yemen yaomba msaada wa mataifa ya Kiarabu dhidi ya Huthi

Serikali ya Yemen imeyataka mataifa jirani ya Kiarabu kuingilia kati kijeshi nchini humo ili kupambana na mashia wa Huthi

Serikali ya Yemen imeyataka mataifa jirani ya Kiarabu kuingilia kati kijeshi nchini humo ili kupambana na mashia wa Huthi. Rais wa Yemen, aliyejiuzuru nakujirudisha tena madarakani Abdu-Rabbu Mansour Hadi, ameuomba Umoja wa Mataifa kupiga marufuku ndege kuruka kutoka kwenye viwanja vya ndege vinavyodhibitiwa na wanaharakati hao wa kishia. Waziri wa Mambo ya nje wa Yemen, Riyadh Yaseen, amezitaka nchi sita wanachama wa Baraza la Ushirikiano la mataifa ya Ghuba, kusaidia kuzuia kusambaa kwa wanaharakati wa kishia wa Houthi, na ameishutumu Iran kwa kuwaunga mkono wanaharakati hao wa kishia.

Mzozo unaoongezeka nchini Yemen kati ya wamaharakati wa kishia wa Huthi na Waislamu wa madhehebu ya Sunni, umeitumbukiza nchi hiyo katika ghasia. Saudi Arabia imetaka ombi la Yemen liungwe mkono, na imesema itachukua hatua madhubuti kuhakikisha inailinda kanda hiyo.

Saudia Arabia ni nchi ya kiislamu inayoongozwa na waislamu wa madhehebu ya Sunni yenye msimamo mkali ambao wanafahamika kama Wahabia, dhehebu hili linahesabika kuwa ni adui mkubwa wa dhehebu la kiislamu la Shia ambalo ni dhehebu la kiislamu lisilo na itikadi za ukatili.

Nchi za kiarabu hasa za kifalme zinahofia kusambaa kwa nguvu za mashia, na kuona kwamba ni hatari kwa mstakabali wa utawala wao wa kifalme.