27 Machi 2015 - 11:05
 Rubani Andreas Lubitz alimzuwia mwenzake kuingia chumba cha rubani na hatimaye kuiangusha ndege

Maafisa wa Ufaransa wanaochunguza ajali ya ndege ya kampuni ya Germanwings iliyoanguka kusini mwa nchi hiyo, wamesema yaonekana rubani msaidizi aliiangusha ndege hiyo kwa maksudi.

Maafisa wa Ufaransa wanaochunguza ajali ya ndege ya kampuni ya Germanwings iliyoanguka kusini mwa nchi hiyo, wamesema yaonekana rubani msaidizi aliiangusha ndege hiyo kwa maksudi.

Rekodi za sauti zinaonyesha kuwa rubani huyo msaidizi Andreas Lubitz alimzuwia nahodha kuingia tena kwenye chumba cha marubani kabla ya ndege hiyo kuanguka kwenye milima ya Alp ya Ufaransa.

Mwendesha mashtaka anaeshughulikia ajali hiyo amesema tafsiri inayoelekea kwenye ukweli zaidi ni kwamba Lubitz alifunga mlango wa chumba cha marubani na kukataa kuufungua.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema jana kuwa habari hizo ziko nje ya uwezo wa kufikiri. Raia 75 wa Ujerumani walikuwemo ndani ya ndege hiyo ya kampuni ya Germanwings, ambayo ni kampuni tanzu ya Lufthanza.