29 Machi 2015 - 11:29
 Magaidi watangaza kuuteka mji muhimu nchini Syria

Muungano wa makundi ya kigaidi yanayodhaminiwa na Israel, Marekani na Saudia arabia kwa lengo la kuiangusha serikali ya Syira wakiongozwa na tawi la Al-Qaeda nchini Syria wamefanikiwa kuchukuwa udhibiti kamili wa mji wa Idlib Jumamosi ya jana

Muungano wa makundi ya kigaidi yanayodhaminiwa na Israel, Marekani na Saudia arabia kwa lengo la kuiangusha serikali ya Syira wakiongozwa na tawi la Al-Qaeda nchini Syria wamefanikiwa kuchukuwa udhibiti kamili wa mji wa Idlib Jumamosi ya jana, hili linatajwa kuwa ni pigo kubwa kwaserikali ya rais Bashar al-Assad, ambaye vikosi vyake vilitoweka kwa kasi baada ya siku nne za mapigano. Magaidi walio pandikizwa na nchi za magharibi wakiwemo kutoka kundi la Al-Nusra wamekuwa wakidhitbi maeneo ya nje ya mji na miji midogo katika mkoa wa Idlib tangu mwaka 2012, lakini vikosi vya Assad viliweza kuimarisha udhibiti wa mji wa Idlib, ulioko karibu na mpaka wa Uturuki, wakati wote wa mgogoro huo. Lakini siku ya Jumamosi, magaidi wote wanaopata udhamini wa Marekani, Israel na Saudia arabia walijiunga na kufanya mashambulizi makali na hatimaye kufanikiwa kuingia  mjini humo, na kuchukuwa udhibiti wa majengo muhimu na kuchana picha za raid Bashar Assad, magaidi hao waliua raia wengi katika mashambulizi hayo ambapo wengi wao ni wanawake na watoto. Licha ya kuwa mji muhimu wa wakazi wapatao 165,000, mji wa Idlib pia uko kwenye njia kuu inayounganisha mji mkuu Damascus na mkoa wa Aleppo. Kwa kuuteka mji huo wa serikali katika ardhi inayodhibitiwa kwa sehemu kubwa na magaidi, kikundi cha Al-Nusra Front kimeimarisha udhibiti wake wa eneo inalolidhibiti kuanzia mpakani mwa Uturuki hadi karibu na miji ya kati ya Syria.

Kwa upande mwingine majeshi ya Syria yameendelea kuwaangamiza magaidi katika miji mbali mbali ya nchi hiyo.

Hapo awali makundi ya kigaidi yanayodhaminiwa na Saudia arabia, Uturuki, Israel, na Marekani yalitangaza kuiangusha serikali ya Syria kwa kipindi kisichozidi miezi sita, lakini majeshi ya Syria yakisaidiwa na vikosi vya makomandoo wa Hizbullah wakiongozwa na wataalam wa vita kutoka Iran, wamefanikiwa kuziharibu ndoto za Marekani na wafuasi wake za kuiangusha serikali ya Syria na sasa imepita miaka mitano, hakuna hata matarajio ya kuiangusha serikali hiyo ya kidemokrasia.