Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA:wazirir mkuu wa Iraq (Haidar Al Abadi) ametangaza rasmi kukombolewa wilaya ya Tikrit ambayo ni makao makuu ya mkoa wa Salahunndini kutoka kwa kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini humo
Televishen ya taifa ya Iraq alasili ya jumanne ilitangaza kukombolewa kikamilifu wilaya hiyo na kusimikwa bendera ya Iraq katika jengo la makao makuu ya wilaya hiyo.
Waziri mkuu wa nchi hiyo ametangaza kuwa jeshi la Iraq likishirikiana na majeshi yakujetulea yawananchi baada ya kuukomboa ubande wa kusini na magharibi ya wilaya hiyo kutoka mikononi mwa kikundi cha Daesh, wamefanikiwa kuunganisha wilaya hiyo na kaskazini mwa mji mkuu wa Iraq Baghdadi.
Naye ametoa shukurani kwa jeshi la Iraq na wananchi waliongana na jeshi hilo katika kuikomboa Iraq na magaidi hao.
Kamanda wa majeshi ya mkoa wa Salahunndini Abdullwahabi Assaidi ametangaza kuwa makundi ya magaidi waliokuwa katika wilaya hiyo wamekimbia kwa makundi, nakusisitiza kuwa baada yakuingia katika makao makuu ya mkoa huo wakuliwa tayari walishakimbia.
Pia viongozi wa mkoa huo wametakiwa kuanzia kesho kwenda maofisini kwaajili ya kuanza kazi rasmi mkoani humo.
31 Machi 2015 - 19:11
Msimbo wa Habari: 680304
Waziri mkuu wa Iraq akibainisha kuwa wilaya ya Tikrit imeshakombolewa na bendera ya Iraq kusimikwa katika jengo la makao makuu ya wilaya hiyo akibainisha kuwa jeshi la Iraq wakishirikiana na jeshi la wananchi wanaendelea kupambana na Daesh katika maeneo mengine yaliobaki