Rais wa Marekani Barack Obama ameachia tena msaada wa kijeshi kwa Misri, ambao ulisitishwa kufuatia mapinduzi dhidi ya serikali iliyochaguliwa mwaka 2013.
Ikulu ya rais mjini Washington imesema rais Obama alimpigia simu mwenzake wa Misri Abdel Fattah al-Sisi jana Jumanne, na kumuarifu kuwa Marekani itaipa Misri ndege 12 za kijeshi aina ya F-16, makombora ishirini pamoja na vifari 125.
Hata hivyo Marekani ilikuwa ikishirikiana na Misri katika operesheni dhidi ya ugaidi. Taarifa ya Ikulu ya Marekani imesema msaada huo wa kijeshi kwa Misri unatolewa kwa maslahi ya usalama wa taifa wa Marekani, na sio utambuzi kwamba Misri imepiga hatua kidemokrasia.