Mamlaka ya Palestina imekuwa mwanachama kamili wa mahakama ya kimataifa inayoshughulikia uhalifu na inaadhimisha tukio hilo muhimu kwa sherehe ndogo katika makao makuu ya mahakama hiyo mjini The Hague.
Palestina imetia saini mkataba ulioanzisha mahakama hiyo mwezi Januari na uanachama wake unaanza rasmi leo, tukio lililokaribishwa na wanaharakati ambao wanaliona tukio hilo kama nafasi ya kuleta uwajibikaji katika miaka kadhaa ya mzozo kati ya Wapalestina na Israel.
Israel si mwanachama wa mahakama ya ICC, lakini jeshi la nchi hiyo pamoja na viongozi wa kiraia wanaweza sasa kukabiliwa na mashtaka iwapo wataaminika kufanya uhalifu ndani ya ardhi ya palestina.
Serikali ya Israel imesikitishwa na hatua ya Palestina hii inatokana na hofu waliyonayo kufuatia jinai, mauaji na ukiaukaji wa haki za binadamu walizozifanya dhidi ya raia madhulumu wa Palestina.