Seneta wa Kentucky nchini Marekani wa chama cha upinzani cha Republican Rand Paul, ametangaza rasmi kuwa atagombea urais katika kile alichokisema ni kurejesha nchi hiyo kwa misingi ya uhuru na serikali ndogo. Paul ambaye anahudumu muhula wake wa kwanza kama seneta kutoka Kentucky ameanzisha kampeini za azma yake ya kuwa Rais katika jimbo lake la Louisville akiwa na ujumbe mkali kwa serikali ya sasa na hata kwa wanasiasa wenzake wa chama cha Republican. Mwanasiasa huyo ni seneta wa pili kutangaza rasmi nia ya kugomeba urais katika uchaguzi mkuu mwaka ujao baada ya Seneta wa jimbo la Texas Ted Cruz kufanya hivyo. Wanasiasa wengine wa chama cha Republican ambao wameonyesha nia ya kugombea urais ni aliyekuwa Gavana wa jimbo la Florida Jeb Bush na Gavana wa jimbo la Wesconsin Scott Walker,ambaye bado hajatoa tamko lake rasmi.
8 Aprili 2015 - 13:46
Msimbo wa Habari: 682014
Seneta wa Kentucky nchini Marekani wa chama cha upinzani cha Republican Rand Paul,