Mwanafunzi mmoja amefariki dunia na zaidi ya wanafunzi mia moja wa chuo kikuu cha Nairobi wamejeruhiwa leo asubuhi baada ya kutokea hitilafu za umeme katika chuo hicho zilizosababisha mlipuko mkubwa uliodhaniwa na wanafunzi hao kuwa shambulizi la kigaidi. Tukio hilo la kulipuka kwa transfoma katika eneo la chuo hicho la Kikuyu lilitokea mwendo wa saa kumi za Alfajiri na kusababisha hali ya taharuki na hofu miongoni mwa wanafunzi. Baadhi ya wanafunzi waliruka kutoka orofa ya sita ya mabweni yao na zaidi ya mia moja wamelazwa katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta na katika hospitali nyingine mjini Nairobi wengine wakiwa katika hali mahututi. Haya yanakuja wiki mbili baada ya wanafunzi 148 wa chuo kikuu cha Garissa kuuawa na waasi wa kundi la Al Shabab.Serikali ya Kenya imeipa Umoja wa Mataifa muda wa miezi mitatu kuihamishia Somalia kambi ya wakimbizi ya Dadaab ilioko Kenya inayowahifadhi zaidi ya wakimbizi nusu milioni wengi wao kutoka Somalia.
12 Aprili 2015 - 11:48
Msimbo wa Habari: 683025
Mwanafunzi mmoja amefariki dunia na zaidi ya wanafunzi mia moja wa chuo kikuu cha Nairobi wamejeruhiwa leo asubuhi baada ya kutokea hitilafu za umeme katika chuo hicho zilizosababisha mlipuko mkubwa uliodhaniwa na wanafunzi hao kuwa shambulizi la kigaidi.